TFS YASHIRIKI KIKAO CHA UWEKEZAJI KUTANGAZA UTALII WA MISITU. Akizungumza kwa niaba ya Kamishina wa Uhifadhi TFS Profesa Dos Santos Silayo tarehe 17/05/2022 jijini Dar es salaam Mhifadhi Mkuu Zainabu Bhungwa amesema kikao hicho kati ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na utalii Mh Juma Selemani Mkomi na Wawekezaji kutoka Ufaransa utaleta tija katika kuutangaza utalii wa Misitu. Bi Zainabu amesema kupitia kikao hicho TFS imepata nafasi ya kuwaeleza wawekezaji hao fursa za uwekezaji kwenye Vivutio vya Utalii vinavyosimamiwa na TFS. "Kikao hiki ni muhimu kwa TFS, tumeweza kuwaeleza Wawekezaji fursa za kuwekeza kwenye Vivutio vyetu, kama ilivyo kwa Mheshimiwa Rais kupitia filamu ya Tanzania The Royal tour anavyotangaza utalii, sisi TFS pia tunamuunga mkono kupitia Vivutio vyetu vya Utalii kwenye Hifadhi za Misitu." Bi Zainabu. Awali katika kikao hicho Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na utalii Mh Juma Selemani Mkomi amewakaribisha wawekezaji hao na kuwahakikishia ku
TUME YA MADINI YAWAPIGA MSASA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI KUHUSU USIMAMIZI WA AFYA, USALAMA, BARUTI NA SHERIA ZA MADINI KWENYE UCHIMBAJI MADINI MIRERANI Timu ya wataalam waandamizi wa Tume ya Madini wakiongozwa na Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Migodi na Mazingira, Mhandisi Henry Mditi wameendelea kutoa mafunzo kwa wamiliki wa migodi, wachimbaji wadogo wa madini na wasimamizi wa baruti kuhusu usimamizi wa afya, usalama, baruti na sheria za madini katika eneo la Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara. Katika mafunzo hayo ambayo awali yamezinduliwa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba mada zilizotolewa ni pamoja na sheria ya madini na kanuni kuhusu eneo tengefu la Mererani na uchimbaji salama migodini. Mada nyingine ni pamoja na utunzaji wa mazingira migodini na usimamizi wa baruti migodini. Wakizungumza katika nyakati tofauti wadau wa madini waliohudhuria mafunzo hayo wameipongeza Tume ya Madini kwa utoaji wa elimu safi na kushauri elimu kuendelea kutolewa kwenye